Virusi vya homa ya ini ni hatari kuliko VVU
11 September 2024, 7:38 pm
Virusi vya ugonjwa wa homa ya ini ni rahisi kuambukizwa kutoka kwa mtu mwenye maambukizi hadi mwingine na kuleta madhara kwa muda mfupi kuliko VVU
Na Yusuph Hassan. Kwa mujibu wa Wizara ya Afya nchini inakadiriwa kiwango cha ushamiri wa ugonjwa wa Homa ya Ini kufikia asilimia 3.5 (aina B) na asilimia 1 (aina C) ilihali barani Afrika kuna Watu milioni 60 wanaishi na maambukizi sugu ya Virusi vya Homa ya Ini aina B na Watu milioni 10 wanaishi na maambukizi sugu ya Virusi vya Homa ya Ini aina C.
Je ni kwa kiwango gani jamii inaelewa juu ya kujikinga dhidi ya ugonjwa wa homa ya ini?
Takwimu za Shirika la Afya Duniani za mwaka 2021 zinaonesha kuwa , kati ya watu wapatao milioni 296 duniani kote wanaishi na maambukizi sugu ya Virusi vya Homa ya Ini aina B na watu takribani milioni 58 wanaishi na maambukizi sugu ya Virusi vya Homa ya Ini aina C.