Dodoma FM

Kelele nyumba za starehe zinakwamisha maendeleo

4 September 2024, 7:03 pm

Halmashauri za nchi zimehimizwa kuandaa muongozo maalumu wa maadili kwaajili ya uendeshaji na usimamizi wa baa na klabu katika maeneo mbalimbali

Kelele nyumba za starehe zinakwamisha maendeleo

Na Mariaam Kasawa. Halmashauri za nchi zimehimizwa kuandaa muongozo maalumu wa maadili kwaajili ya uendeshaji na usimamizi wa baa na klabu katika maeneo mbalimbali. Hii ni moja kati ya mapendekezo matano yaliyo tolewa na washiriki wa Tamasha la 7 la jinsia ngazi ya wilaya – Wayani Kondoa .

Mwenyekiti wa Bodi ya mtandao wa jinsia Tanzania TGNP  Bi. Gemma Akilimali anasema ukosefu wa miongozo thabiti kwa wamiliki na wasimamizi wa sehemu za starehe  ni kikwazo cha kufikia maendeleo endelevu.

Sauti ya Bi. Gemma Akilimali

Aidha amewataka wanajamii, vikundi na vituo vya taarifa na maarifa kushirikiana kwa pamoja kuripoti vitendo vya ukatili wa kijinsia hususani kipindi hi ambacho nchi inaelekea katika uchaguzi.

Sauti ya Bi. Gemma Akilimali