Dodoma FM

Vipimo ni muhimu kwa thamani halisi ya pesa ya mteja

3 September 2024, 5:13 pm

Mikakati inayofanywa na wakala wa vipimo ikiwemo utoaji wa elimu kwa jamii juu ya vipimo sahihi pamoja na kufanya ukaguzi wa vipimo vya huduma mbalimbali.

Na Fred Cheti.

Wananchi Jijini Dodoma wameshauriwa kuhakiki vipimo sahihi vya bidhaa au huduma mbalimbali wanazopatiwa ili kupata huduma au bidhaa inayoendana na thamani halisi ya malipo ya pesa.

Hayo yameelezwa na Meneja wa Wakala wa Vipimo Mkoa wa Dodoma Bw. Karimu Zuberi wakati akifanya mahojiano na Dodoma TV kuhusu umuhimu wa jamii kuzingatia huduma za vipimo sahihi.

Sauti ya Bw. Karimu Zuberi

Aidha Meneja huyo ameeleza mikakati inayofanywa na wakala huo ikiwemo utoaji wa elimu kwa jamii juu ya vipimo sahihi pamoja na kufanya ukaguzi wa vipimo vya huduma mbalimbali.

Sauti ya Bi. Merisiana Lucas

Aidha kwa upande mwingine wanachi wa Dodoma wamekuwa na maoni tofauti kuhusiana na uelewa wao juu ya vipimo sahihi kwa bidhaa au huduma mbalimbali wanazopata na wanashauri nini kifanyike.

Sauti ya Bw. Maiko Peter

Wakala wa Vipimo mara kwa mara imekuwa ikiwataka wafanyabiashara na wajasiriamali wote kuzingatia matumizi sahihi ya vipimo katika uuzaji na ufungashaji wa bidhaa zao ili kuhakikisha hawajipunji na hawawapunji wanunuzi wa bidhaa zao kwani kwa kufanya hivyo pande zote mbili zitaendelea kunufaika na kukuza uchumi wa biashara zao na uchumi wa nchi kwa ujumla.