Dodoma FM

Jeshi la polisi lamshikilia mmoja kifo cha msanii Man Dojo

13 August 2024, 3:23 pm

Mtu huyo anashikilwa kwaajili ya mahojiano ya tukio hilo.Picha na BBC.

Watu Wawili wilayani Bahi wameuwawa baada ya kushambuliwa sehemu mbalimbali na kuchomwa moto katika gari .

Na Seleman Kodima.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linamshikilia RAPHAEL KENETH NDAMAHNUWA, mwenye umri wa miaka 26 Mkazi wa Nzuguni B kwa ajili ya mahojiano kuhusu Tukio la kifo cha Msanii Joseph Francis Michael maarufu Man Dojo.

Akizungumza juu ya tukio hilo Kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma SACP Anania Amo amesema mnamo tarehe 11 mwezi wa nane mwaka huu majira ya saa 11 alfajiri Msanii Joseph fransis maarufu Mandojo alikutwa ndani ya uzio wa kanisa katoliki Parokia ya Watakatifu wote akiwa amejificha katika Banda la Mbwa.

Sauti ya SACP Anania Amo .

Aidha Katika tukio linguine Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limesema kuwa watu Wawili wilayani Bahi wameuwa baada ya kushambuliwa sehemu mbalimbali na kuchomwa moto katika gari .

SACP Anania amesema tukio hilo limetokea August 10 mwaka huu Majira ya saa nne usiku katika kitongoji cha Juhudi kata ya Ibihwa wilayani Bahi ambapo watu wawili FRANCO FILBERT MTASOKA, Mwenye umri wa Miaka 29, ambaye ni , Dereva, Mkazi wa Kisasa na RAMADHAN ABEID, mwenye umri wa Miaka 27, wameuawa kwa kushambuliwa sehemu mbalimbali za miili yao na kisha kuchomwa moto ndani ya gari namba T. 583 BEW aina ya Toyota Cresta na baada ya wananchi kujichukulia sheria mkononi.

Sauti ya SACP Anania Amo .