Dodoma FM

Wananchi wapo tayari kujiandika daftari la kudumu la wapiga kura

1 August 2024, 4:25 pm

Picha ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Ramadhani Kailima.Picha na NEC.

Uandikishaji wa daftari la Wapiga kura kwa Mkoa wa Dodoma unatarajiwa kufanyia tarehe 11 hadi 17 Desemba mwaka huu.

Na Pius Jayunga.
Baadhi ya Wakazi wa Dodoma wameeleza kuwatayari kushiriki katika zoezi la kujiandikisha katika daftari la kudumu la Wapiga ambalo linatarajiwa kufanyika mapema mwezi Desemba katika Mkoa wa Dodoma.

Wakizungumza na Dodoma Tv kwa nyakati tofauti Wananchi hao akiwemo Idan Jailos, wamesema kutokana na jukumu la kupigia kura Viongozi kuwa ni haki yao hivyo kupitia zoezi la uandikishaji wa wapiga kura katika daftari la kudumu la wapiga itawawezesha kwenda kuchagua Viongozi wanaowataka.

Sauti za wananchi.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa yua Uchaguzi, Ramadhan Kailima (kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Uandikishaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura na Tehama, Geofrey Mpangala .Picha na Michuzi.

Kwa upande wake Badru Rajabu kutoka Shirika la Vijana la Restless Development amesema Taasisi hiyo imebeba jukumu la kuwahamsisha Vijana kushiriki katika Uchaguzi Mkuu ujao hasa wale ambao itakuwa ni mara yao ya kwanza kushiriki upigaji kura.

Sauti ya Badru Rajabu.

Akizindua zoezi uboreshaji wa daftari la kudumu la Wapiga kura july. 20 mwaka huu Mkoani Kigoma, Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa alisema Wapiga kura wapya 5,586433 wataandikishwa katika daftari la kudumu la kudumu la Wapiga kura.

Sauti Mh. Kassim Majaliwa .