Dodoma FM

Namna gani tunaweza kumlinda msichana mwenye ulemavu kuepuka mimba za utotoni

8 July 2024, 5:03 pm

Chini ya miaka 18 msichana bdo hajakomaa kiakili na kimwili kuweza kubeba majukumu ya malezi.Picha na Google.

Leo tunaangazia kwa namna gani tunaweza kuwalinda wasichana wenye ulemavu kuepukana na Mimba za utotoni,Mwenzetu Selemani Kodima ametuandali taarifa ifuatayo.

Na Seleman Kodima.
Tatizo la mimba za utotoni limekuwa kubwa duniani na linaongezeka siku hadi siku hasa katika jamii ya uchumi wa chini.

Wataalamu wa afya ya uzazi wanashauri ili kuepukana na matatizo ya kiafya ni vyema kupata mimba baada ya kufikisha umri wa miaka 18.

Chini ya miaka 18 msichana bdo hajakomaa kiakili na kimwili kuweza kubeba majukumu ya malezi,pia nyonga huwa changa na nyembamba hivyo kutoweza kubeba kiumbe na kusababisha madhara makubwa wakati wa kujifungua.