Dodoma FM

Watumishi wa Umma wahimizwa matumizi ya TEHAMA

20 June 2024, 1:01 pm

Picha ni watumishi mbalimbali wa umma wakiwa katika ufunguzi wa wiki ya utumishi wa umma katika viwanja vya Chinangali Park.Picha na George John.

Maonesho haya yanalenga kutoa huduma kwa wananchi moja kwa moja na kwa urahisi zaidi na kupitia maonesho haya serikali inapata maoni kutoka kwa wadau na wananchi kwa urahisi zaidi.

Na Mariam Kasawa.
Watumishi wa umma wametakiwa kuwa wafuatiliaji wa teknolojia mbalimbali za mawasiliano ikiwemo simu ili kufahamu huduma mbalimbali zinazo tolewa na serikali.

Hayo yamebainishwa June 19 katika ufunguzi wa wiki ya utumishi wa Umma na waziri wa Nchi ofisi ya rais utumishi wa umma na utawala Bora Mh. George Simbachawene amesema siku hii hufanyika ili kupima mafanikio na changamoto zinazo zikabili sekta za umma pamoja na kitatua changamoto zinazo zikabili jamii.

Ameongeza kuwa Taasisi zinapaswa kubadilishana uzoefu na Kupata maoni kutoka kwa wadau mbalimbali pamoja Taasisi Kuondoa kasoro za kiutendaji.

Sauti ya Mh. George Simbachawene .
Picha ni Bi Fatma Mohamed Afisa huduma kwa wateja kutoka shirika la umeme Tanzania TANESCO.Picha na George John.

Naibu waziri ofisi ya rais utumishi wa umma na utawala Bora; Ridhiwan Kikwete anasema maonesho haya mwaka huu kwaTaasis za umma yanafanyika kwa aina mbili.

Sauti ya Mh.Ridhiwan Kikwete .

Kwa upande wake Bi Fatma Mohamed Afisa huduma kwa wateja kutoka shirika la umeme TANESCO hapa anaeleza matumizi ya mfumo wa Tehama kwatika manunuzi ya LUKU .

Sauti ya Bi Fatma Mohamed.