Dodoma FM

Wanafunzi vyuo vikuu wachuana uandishi wa insha za usalama barabarani

13 June 2024, 11:41 am

Picha ni Washirika hao kutoka chuo kikuu cha Dodoma wakipatiwa vyeti na aliye kuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo. Picha na Mariam Kasawa.

Kwa mujibu wa taarifa za Shirika la Afya Duniani (WHO), ajali za barabarani ni miongoni mwa sababu namba moja ya vifo kwa watoto wa umri kati ya miaka 5 hadi 14 pamoja vijana wa umri kati ya miaka 15 hadi 29 ambao ndiyo nguvu kazi ya Taifa.

Na Mindi Joseph

Mashindano ya uandishi wa Insha juu ya usalama barabarani kwa wanafunzi wa vyuo vikuu yamefanyika jijini Dodoma na kuibua washindi watano ambao wamepatiwa zawadi.

Kwa mujibu wa shirika la Afya Duniani watu 3,700 hufa kila siku kutokana na ajali za Barabarani kwa kulitambua hilo shirika  la global youth coalition kwa kushirikiana na shirika la  human Dignity and Environmental care Foundation wameanzisha mashindano ya insha kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kwa lengo la kuzungumzia na kuwakumbusha kuhusu usalama barabarani.

Mwenyekiti wa Usalama Barabarani Kanda ya Kati Gasper Kisenga anasema tabia mbaya za uendeshaji wa vyombo vya moto vinachangia ajali.

Picha ni mgeni rasmi katika hafla hiyo ambeye pia ni Mwenyekiti wa Usalama Barabarani Kanda ya Kati Gasper Kisenga akiongea na washiriki hao.Picha na Mariam Kasawa.
Sauti ya Dkt. Gasper Kisenga

Mhandisi Marwa Chacha kutoka Wizara ya Uchukuzi anasema shindano hili linalenga kupunguza ajali za barabrani.

Sauti ya Mhandisi Marwa Chacha.

Washiriki wa Shindano hilo kutoka vyuo vikuu na maafisa usafirishaji marufu kama bodaboda wanasema watakuwa mabalozi kuzuia ajali za barabarani

Sauti za baadhi ya washiriki.
Mratibu wa shughuli za Vijana kutoka shirika la Hudefo Abdi Halifa akiongea na Dodoma Tv.

Abdi KHalifa Mratibu wa shughuli za Vijana wa shirika la Hudefo ambao ni watekelezaji wa mradi wa Bodaboda salama anasema wanaothirika sana na ajali za barabarani ni watu wa rika la kati.

Sauti ya Bw. Abdi Khalifa