Wabunge wapigwa msasa mfumo mpya wa ununuzi wa umma wa kielektroniki NEST
10 June 2024, 7:16 pm
Ikumbukwe kuwa MAMLAKA ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) umeanzisha mfumo mpya wa manunuzi wa kielekroniki National e-Procurement System of Tanzania (NeST) utakaosaidia kudhibiti rushwa, mchakato wa zabuni kuchelewa na kuongeza uwazi wa zabuni .
Na Seleman Kodima.
Wito umetolewa kwa Wabunge kuwa Vinara wa uhamasishaji wa matumizi ya kuhusu mfumo mpya wa ununuzi wa umma wa kielektroniki NEST kwa Wananchi .
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,ajira ,vijana na watu wenye ulemavu Patribas Katambi wakati Akizungumza kwenye semina ya Wabunge iliyoandaliwa na Mamlaka ya udhibiti wa ununuzi wa Umma (PPRA) ambapo amesema ni muhimu Wabunge kuwa sehemu ya utoaji wa elimu hiyo ili wananchi wafahamu thamani halisi ya Miradi ya maendeleo .
Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa PPRA Eliakimu Maswi amesema mfumo huo wa NeST utaanza kutumika rasmi June 17 huku kanuni zake zikitarajiwa kuanza kutumika July mosi mwaka huu.