Dodoma FM

Vijana waonywa wizi wa misalaba makaburi ya Chang’ombe

3 June 2024, 5:09 pm

Picha ni Kaburi ambalo limeharibiwa na kuchuliwa mikanda ya pembeni ya vigae vya sakafu na wezi hao. Picha na Mariam Kasawa.

Makuburi ni mahala pa mapumziko ya milele kwa wafu na ni vyema jamii ikaacha tabia ya kuiba misalaba na mikanda ya vigae vya sakafu.

Na Mindi Joseph.
Wizi wa misalaba ya chuma katika Makuburi yaliyopo kata ya chang’ombe Jijini Dodoma umekithiri jambo ambalo linachochewa na biashara ya vyuma chakavu.

Wakati wananchi wakiomboleza kuwapoteza wapendwa wao na kuwasitiri vyema kwa kujenga makaburi na kuweka misalaba juu yake kulingana na imani zao, baadhi ya watu wamekuwa na ujasiri wa kuiba misalaba hiyo.

Misalaba inayolengwa zaidi ni ya chuma na hata ile iliyo miminiwa ndani yake bado imekuwa ikivunjwa na kuchukuliwa nondo ambazo huuzwa kama chuma chakavu na hapa wananchi wanansema.

Sauti za wananchi

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Mtaa wa Mazengo kata ya chang’ombe Abdallah Mtosa amekemea tabia hiyo huku akisema hatua kali zitachukuliwa kwa vijana na watu wanaofanya vitendo hivyo.

Sauti ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Mazengo kata ya chang’ombe.