Dodoma FM

Mchakato wa uchaguzi wa NaCoNGO ngazi ya Mkoa kuanzia Leo June 3.

3 June 2024, 8:42 am

Mwenyekiti wa kamati ya Mpito ya kuratibu uchaguzi Christina Kamili Ruhinda akiongea na waandishi wa habari Jijini Dodoma.picha naMariam Kasawa.

Uchaguzi huo unakuja kufuatia Baraza lililopo madarakani kumaliza muda wake wa miaka mitatu kikatiba ifikapo Juni 30, 2024.

Na Mindi Joseph

Kamati ya Mpito ya Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NaCoNGO) imetangaza mchakato wa uchaguzi wa wa baraza ngazi ya Mkoa utakaofanyika kuanzia June 3.
Uchaguzi huu utaenda pamoja na uchaguzi wa mashirika yasiyo ya kiserikali kimataifa na wawakilishi wa makundi maalum[ Watoto vijana na watu wenye ulemavu]
Akizungumza leo jijini Dodoma Mwenyekiti wa kamati ya Mpito ya kuratibu uchaguzi Christina Kamili Ruhinda ametangaza ratiba ya uchaguzi huo.

sauti ya Mwenyekiti wa kamati ya Mpito ya kuratibu uchaguzi Christina Kamili Ruhinda

Katibu mkuu kamati ya Mpito ya kuratibu uchaguzi Baraza la Taifa la (NGOs) Ismail Biro anasema baraza hili linateuliwa kwa mujibu wa sheria.

sauti ya Katibu mkuu kamati ya Mpito ya kuratibu uchaguzi Baraza la Taifa la (NGOs) Ismail Biro