CAG awasilisha ripoti kwa Rais Dkt. Samia Suluhu
28 March 2024, 6:52 pm
Deni hilo linajumuisha deni la ndani Shilingi Trilioni 28.92 deni la nje Shilingi Trilioni 53.32.
Na Seleman Kodima.
Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa serikali (CAG) Charles E. Kichere, amesema kuwa deni la Serikali hadi kufikia Juni 30, 2023 lilikuwa Shilingi Trilioni 82.25 ni sawa na ongezeko la 15% kutoka Shilingi Trilioni 71.31 kwa mwaka 2021/22.
Hayo ameyasema leo wakati anakabidhi ripoti ya CAG kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan katika Ikulu ya Chamwino Jijini Dodoma .
Aidha Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa serikali ameeleza kuwa kampuni ya ndege Tanzania (ATCL), imepata hasara ya Shilingi Bilioni 56.64 sawa ongezeko la 61% kutoka hasara ya shilingi bilioni 35.24 kwa mwaka uliopita.