Wananchi waelezea mafanikio ya miaka mitatu ya Rais samia
20 March 2024, 7:04 pm
Ni takribani miaka mitatu imepita tangu kuapishwa kwa rais wa wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh samia Suluh Hasan Tareh 19 machi mwaka 2021.
Na Thadei Tesha.
Wananchi jijini Dodoma wamelezea mafanikio ya miaka mitatu ya uongozi wa serikali ya awamu ya sita chini ya rais Dk Samia Suluh Hasan Tangu kuingia madarakani.
Safari ya uongozi wa rais Dkt Samia suluhu Hasan ilianza rasmi ingawa baadhi ya watu walikuwa na mashaka kwani ndiye rais wa kwanza mwanamke kuwahi kutokea hapa nchini,lakini kujiamini kwake kulindoa baadhi ya minongono kupitia kauli hii.
Baada ya kauli hii ndipo safari ya kuanza kazi ya kuwatumikia watanzania ilianza rasmi miradi mbalimbali iliyoachwa na awamu iliyopita ikikamilishwa huku mingine iianzishwa.
hawa ni wkazi wa jiji la Dodoma wakiendelea na shughuli zao za kila siku wanasema kuwa miaka mitatu ya uongozi wa Rais Dkt Samia Suluh Hasan imesaidia kuleta maendeleo katika sekta mbalimbali.
Lakini gharama za maisha ni moja ya changamoto ambazo wananchi wanatoa wito kwa serikali kuzidi kuliangalia.
Tarehe 19 ya mwezi machi ni tarehe ambayo Taifa la Tanzania liliandika Historia ya kupata rais wa kwanza mwanamke ambapo kauli kama mama anaupiga mwingi,mama ukimzingua anakuzingua kazi iendelee ni kauli zinazodhihirisha utendaji wa kazi.