Wakulima wapatiwa elimu ya kukabiliana na mvua nyingi
31 January 2024, 7:59 am
Mifugo na baadhi ya mazao hutegemea ufanisi wa wataalamu hususani inapokuja mabadiliko ya hali hewa hivyo ni vyema kufuata ushauri wataalamu wa kilimo pamoja na mifugo.
Na Victor Chigwada .
Wakulima na wafugaji wa kata ya Handali wilaya ya Chamwino wameendelea kupewa elimu juu ya namna bora ya kukabiliana na mvua nyingi mashambani pamoja na kuilinda mifugo dhidi ya kupe katika msimu huu wa masika.
Daudi Kolokoni ni Afisa kilimo na mifugo kutoka Handali amesema endapo wakulima watafuata njia sahihi za kilimo itawapa fursa ya mavuno ya kutosha.
Kolokoni amesema kuwa wamewahimiza wakulima kulima mazao rafiki yatakayo himili hali hewa pamoja na kulima kwa kuweka matuta ambayo yatawasaidia kuvuna maji yanayo tiririka mashambani.
Aidha kwa upande wa wafugaji nao wameaswa kujiandaa kukabiliana na magonjwa yatokanayo na wadudu kama kupe.
Amesema kuwa ni vyema wafugaji kuhakikisha wanapeleka mifugo yao mahala pa josho au kutumia njia ya kunyunyizia matone na kuondokana na sababu za kukosekana kwa josho ndani ya Kata