Dodoma FM

Zoezi la uzoaji taka lasuasua baadhi ya maeneo Jijini Dodoma

31 January 2024, 7:36 am

Picha ni taka zikiwa zimerundikwa katika eneo ambalo sio rasmi zikisubiri kubebwa na gari la taka.Picha na Thadei Tesha.

Ni hivi karibuni Dodoma Tv iliripoti uwepo wa mkusanyiko wa taka katika maeneo mbalimbali ikiwemo eneo la Nyerere square.

Na Thadei Tesha.

Kuharibika kwa magari ya kuzolea taka katika maeneo mbalimbali Jijini Dodoma imetajwa kuwa miongoni mwa sababu inayochangia baadhi ya maeneo kusuasua kwa zoezi la uzoaji taka.

Dodoma tv imefanya mahojino maalum na afisa Afya wa Jiji la Dodoma anayehusika na suala la uzoaji wa taka katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dodoma Bw Job Steven hii ni kufuatia uwepo wa mrundikano wa taka kwa muda mrefu katika baadhi ya maeneo kukaa kwa muda mrefu bila ya kuzolewa.

Hapa anaeleza sababu inayopelekea suala la uzoaji wa taka katika baadhi ya maeneo hayo ikiwemo eneo la Nyerere square kuwa wa kusuasua.

Sauti ya Bw Job Steven .
Picha ni Afya wa Jiji la Dodoma anayehusika na suala la uzoaji wa taka katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dodoma Bw Job Steven .Picha na Thadei Tesha.

Lakini hapa anatioa wito kwa wananchi juu ya suala la uhifadhi wa mazingira kwa kuepuka kutupa taka hovyo ikiwa ni pamoja na suala la kulipa ada ya uzoaji wa taka kwa wakati.

Sauti ya Sauti ya Bw Job Steven .

Ni hivi karibuni Dodoma Tv iliripoti uwepo wa mkusanyiko wa Taka katika maeneo mbalimbali ikiwemo eneo la Nyerere square ambapo wananchi wanasema kuwa taka hizo zinakaa kwa muda mrefu bila ya kuzolewa.

Sauti za wananchi.