Aweso aitaka Duwasa kumaliza tatizo la maji UDOM
23 January 2024, 8:00 pm
Kwa mujibu wa makamu mkuu wa chuo kikuu cha Dodoma UDOM anasema chuo hicho kinakadiriwa kuwa na wanafunzi takribani elfu 36 hivyo kuchangia ongezeko la uhitaji wa huduma ya maji katika chuo hicho.
Na Thadei Tesha.
Waziri wa maji mh Juma Aweso ametoa maagizo kwa viongozi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Duwasa kuhakikisha inaweka mikakati ya kuwezesha kuondoa tatizo la maji katika chuo kikuu cha Dodoma (UDOM)
Waziri Juma Aweso ameyasema hayo wakati akizungumza na viongozi wa chuo kikuu cha Dodoma UDOM pamoja na viongozi kutoka mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Duwasa.
Amesema ni wakati wa viongozi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Duwasa kushirikiana na wizara hiyo pamoja na wataalamu kutoka chuoni hapo ili kuweka mikakati kuondoa changamoto ya maji chuoni hapo.
Lakini je hali ya upatikanaji wa maji katika chuo kikuu cha Dodoma ipoje kwa sasa? Huyu hapa Makamu Mkuu wa chuo kikuu cha Dodoma anaeleza hali ilivyo kwa sasa.