Dodoma FM
Washiriki 1,707 wajiandikisha kushiriki utoaji maoni
11 January 2024, 6:58 pm
Baada ya hapo, kamati hiyo itachambua maoni hayo yaliyopokewa.
Na Seleman Kodima.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Joseph Mhagama amesema jumla ya washiriki 1,707 wamejiandikisha kwenye ushiriki wa utoaji maoni.
Pia, taasisi za kidini, mashirika manne, vyama vya siasa 18, taasisi na asasi za kiraia 31 zimeshiriki huku wachangiaji binafsi 68 wakitoa maoni yao.
Mhagama amesema hayo jana bungeni jijini Dodoma wakati akihitimisha utoaji wa maoni uliodumu kwa siku nne.