Ndugai akerwa na wanafunzi wanaojifelisha darasa la saba
9 January 2024, 9:01 pm
March 14 mwaka 2023 Halmashauri ya wilaya ya Kongwa kupitia kwa mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo white zuber ilitangaza kuanza kuwanunulia mahitaji yote ya msingi wanafunzi wenye wazazi wasiojiweza kiuchumi watakaofaulu na kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza.
Na Pius Jayunga.
Spika mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Kongwa Mhe. Job Yustino Ndugai amekemea tabia ya baadhi ya wazazi kuwashawishi watoto wao kujifelisha masomo kwa lengo la kuajiriwa kazi za ndani.
Mhe. Ndugai amekemea tabia hiyo wakati akizungumza na wadau wa elimu wakiwemo wazazi na walezi wa wahtimu wa darasa la saba mwaka 2023 waliofeli mitihani kinyume na matarajio.
Mh. Ndugai amewataka wazazi wilayani Kongwa kuacha mara Moja vitendo hivyo.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Mayeka Simon Mayeka, ameagiza wanafunzi waliofeli mtihani wa darasa la Saba mwaka 2023 kinyume na matarajio kurudia darasa hilo ili kutimiza azma ya Serikali ya Kuifanya elimu ya kidato cha nne kuwa ya lazima.
Amewataka wazazi na walezi kutambua thamani ya elimu kwa watoto wao na kuepusha matumizi athari za kiuchumi kutokana na tabia ya kushawishi watoto kufanya vibaya katika mithani yao.