Mrundikano wa taka soko la samaki Bonanza wahatarisha afya za wananchi
20 December 2023, 4:43 pm
kwa mujibu wa wafanyabiashara wa soko hili wanadai ni muda mrefu tangu kuanza ujenzi wa soko hili na iwapo litakamilika linatarajiwa kupunguza athari mbalimbali wanazopitia wafanyabiashara hao.
Na Thadei Tesha
Wafanyabiashara wa soko la Bonanza Jijini Dodoma wameulalamikia uongozi wa Jiji la Dodoma kwa kuchelewa kukamilika kwa mradi wa soko jambo linaloweza kusababisha athari za magonjwa ya mlipuko hususani kipindi hivi cha mvua.
Dodoma tv imefika katika soko hili nakushuhudia mbali na shuguhli za kuuza samaki zikiendelea, mazingira ya soko hili bado si rafiki hivyo kuwalazimu wafanyabiashara hawa kuuza bidhaa zao wakiwa wamepang chini licha ya wadudu kuonekana wakizagaa maeneo hayo.
Inaelezwa kuwa ni muda mrefu tangu ujenzi wa soko jipya la samaki ufanyike katika eneo hili lakini hadi sasa bado halijakamilika je, uongozi wa soko hili wamechukua hatua gani?
Inanilazimu kufunga safari hadi katika ofisi ya mkurugenzi wa jiji la dodoma kwa ajili ya kutolea ufafanuzi wa kina juu ya suala hili.
Bw abeid Msangi ni kaimu mkuu wa divisheni ya viwanda na biashara katika jiji la Dododma hapa anaeleza mikakati ya jiji kuboresha miundombinu ya soko hilo.