Jiji la Dodoma kutoa milioni 20 katika kituo jumuishi
20 December 2023, 2:31 pm
Kongamano hilo la wadau wa Elimu jumuishi katika Mkoa wa Dodoma limewakutanisha watu mbalimbali wakiwemo maafisa elimu kata ,wazazi ,viongozi wa dini pamoja na wafadhili wa baadhi ya Miradi katika vituo jumuishi vilivyopo jijini hapa huku kauli mbiu katika kongamano hilo ikiwa ni ”FURSA SAWA YA ELIMU KWA MTOTO MWENYE ULEMAVU NA MTOTO WA KIKE”.
Na Mariam Matundu.
Halmashauri ya jiji la Dodoma imepanga kutoa kiasi cha shilingi milioni 20 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya kufundishia katika kituo jumuishi cha utoaji wa elimu kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu kilichopo katika shule ya Msingi Nkuhungu jijini hapa
Hayo yameelezwa leo na Afisa Elimu maalumu katika jiji la Dodoma Bwana Issa Kambi wakati akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa jiji la Dodoma katika Kongamano la wadau wa Elimu jumuishi katika Mkoa wa Dodoma lililoandaliwa na Kanisa la FPCT lililofanyika katika shule ya Mtemi Mazengo jijini hapa.
Kwa upande wake Mratibu wa Mradi wa Elimu jumuishi katika halmshauri za wilaya ya Dodoma na Bahi Bi Jane Mgindange anazungumzia lengo la kuwa na kongamano hilo la wadau wa elimu jumuishi pamoja na hali ya maendeleo ya Elimu jumuishi katika wilaya hizo mbili.
Kwa upande wao walimu na wazazi na watoto wanasoma katika vituo hivyo nao walikua na haya ya kuzungumza.