Dodoma watakiwa kuchukua tahadhari dhidi ya mvua zinazoendelea
6 December 2023, 12:20 pm
Mvua zinazoendelea kunyesha nchini zinatajwa kusababisha madhara mbalimbali ikiwemo vifo vya watu 63 vilivyotokea katika wilaya ya hanag mkoani manyara usiku wa kuamkia jumapili ya nov. 03 mwaka huu.
Na Thadei Tesha.
Kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha mafuriko katika baadhi ya maeneo nchini, wakazi jijini Dodoma wametakiwa kuchukua tahadhari dhidi ya mvua hizo.
Meneja wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Kanda ya kati Bw. Isdory Kilenga amezungumza na kituo hiki na kuwasihi wakazi wa jiji la dodoma kuchukua tahadhari dhidi ya maafa hayo.
Amesema tahadahri moja wapo wanayopaswa kuchukua ni pamoja na kuhama kutoka maeneo ambayo yaa asili ya maji kutuhama na kuepuka kutumia vifaa vya umeme pindi mvua zinaponyesha ili kuepukana na madhara yatokanayo na mvua.
Nao baadhi ya wananchi jijini dodoma wametoa maoni yao juu ya tahadhari wanazochukua ikiwemo kusikiliza maelekezo yanayotolewa na mamlaka ya hali ya hewa ili kuepukana na maafa hayo