TAMWA yahimizwa kuweka mkazo ajenda ya uhuru wa kujieleza
30 November 2023, 2:57 pm
(TAMWA) tunaahidi kumuunga mkono kivitendo kwa sababu ni jukumu ambalo tumealianza tangu miaka 36 iliyopita.
Na Alfred Bulahya.
Chama cha wahandishi wa habari wanawake Tanzania (TAMWA) kimetakiwa kuweka mkazo mkubwa katika uhuru wa kujieleza unaojumuisha sauti za wanawake ndani ya ajenda ya jumla ya haki za binadamu.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama wakati alipomuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan katika maadhimisho ya miaka 36 ya chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
Waziri, ametoa wito kwa (TAMWA) kuona umuhimu wa mijadala yenye mlengo wa kijinsia na uhusiano kati ya uhuru wa vyombo vya habari, ulinzi na usalama wa waandishi wa Habari wanawake, na uhuru wa kujieleza kuwa kitovu cha kufanya maamuzi katika ngazi ya jamii kitaifa, na kimataifa.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Technolojia ya Habari Bw, Selestine Gervas Kakele amesema inatambua Mchango wa (TAMWA) na wakati wote serikali itaendelea kuangalia ujumbe ambao TAMWA na asasi nyingine inatoa.
Awali Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania (TAMWA) Bi, Joyce Shebe amemshukuru Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kukubali mwaliko.