Polisi wanawake watakiwa kutafuta fursa kufikia malengo
30 November 2023, 2:00 pm
Jeshi la polisi mkoani Dodoma linashiriki katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia duniani zilizoanza novemba 25 na zinatarajiwa kufikia tamati Disemba 10.
Na Arafa Waziri.
Maofisa wa Jeshi la Polisi wanawake Mkoani Dodoma wametakiwa kufanya kazi kwa bidiii na kutafuta fursa ili kufikia malengo ya hamsini kwa Hamsini.
Hayo yamesemwa na Naibu Kamishna wa Polisi Tanzania Marry Nzuki katika kongamano la mtandao wa polisi wanawake lililofanyika jijini dodoma ikiwa ndani ya siku 16 za kupinga ukatili.
Bi marry amesema kuwa kufanya hivyo kutasaidia kujitegemea na kufikia malengo yao pamoja na kuepuka vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Kwa upande wake kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Martin Otieno amesema kutokana na jitihada zilizofanyika zimesadia kupunguza vitendo ya ukatili wa kijinsia dodoma.
Awali akitoa salamu za ukaribisho kwa upande wa jeshi la zimamoto na uokozi mrakibu wa jeshi hilo Rehema Jeremiah ameishauri jamii kupinga vitendo vya ukatili kwa ujumla pamoja na vile vinavyogharimu Maisha ya watu.