Wanawake watakiwa kujikita katika nyanja za siasa
29 November 2023, 4:42 pm
Maadhimisho hayo yamehitimishwa leo Nov 29 Jijini Dar es salaam .
Naibu Waziri wa Habari Kundo Mathew amesema matamanio yake ni kuona wanawake wapo katika nyanja za kisiasa kama ilivyo kwa rais Dkt Samia Suluhu Hassan
Ameyasema hayo Nov 28, 2023 katika maadhimisho ya miaka 36 ya Chama cha Wanahabari Nchini [TAMWA] yanayofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere
Aidha ameongeza kuwa rais anatambua mchango wa TAMWA katika masuala ya wanawake na tasnia ya Habari hivyo Serikali ipo pamoja nao katika yale ambayo wanataka serikali iyafanyie kazi
Awali akiwasilisha ripoti ya utafiti juu ya masuala ya rushwa ya ngono na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia katika vyombo vya habari uliofanyika Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA Dkt Rose Reuben amesema kuwa kuna unyanyasaji wa Kingono amabo wamekuwa wakiukemea kwani wanaamini unapunguza weredi kwa waandishi
Ameema utafiti huo ulihusisha vyombo 17 na wanahabari 137 Tanzania na Zanzibar, katika huo utafiti asilimia 59 waliripoti kuwa wanapitia unyanyasaji huo ndani ya vyombo vya habari.