Asilimia 11 ya akina mama nchini hujifungua kabla ya wakati kila mwaka
19 November 2023, 10:53 am
Siku ya watoto waliozaliwa kabla ya wakati ilianzishwa kwa nia ya kuelimisha kuhusu kujifungua watoto ambao bado hawajakomaa.
Na Mindi Joseph.
Maadhimisho ya siku ya watoto wanozaliwa kabla ya wakati yalifanyika Nov 17 katika hospital ya benjamini mkapa yakiwa yamebeba kauli mbiu isemayo Vitendo vidogo, matokeo makubwa.
Akizungumza na waandishi wa habari mkurugenzi wa hospital ya benjamini mkapa Dr. Alphonce Chandika amesema serikali imeamua kuwekeza katika dawa, vifaa tiba na kuwasomesha wahudumu wa afya ili kupata wataalamu na kuokoa maisha ya watoto
Nae mkurugenzi msaidizi idara ya watoto kutoka hospital ya benjamini mkapa Dr. Julieth Lubengula ameeleza sababu zinazosababisha mama kujifungua mtoto kabla ya wakati
Kwa upande wao baadhi ya wakina mama waliojifungua kabla ya wakati (watoto njiti) ambao watoto hao wanaendelea vizuri wanasema watoto hao ni sawa na watoto wengine wanao zaliwa kwa njia ya kawaida
Takwimu zinaonyesha kuwa takribani wakina mama milioni 2 sawa na asilimia 11 wanajifungua kabla ya wakati vilevile takribani watoto elfu hamsini wenye umri chini ya siku 28 hufariki kutokana na changomoto ya kuzaliwa kabla ya wakati