Ifahamu Miswada mitatu iliyo wasilishwa bungeni wiki iliyopita
15 November 2023, 5:31 pm
Yapo mambo mazuri waliyobaini baada ya Miswada hiyo kuwasilishwa Bungeni ikiwa ni pamoja na vyama vya Siasa kuwa na Sera ya mambo ya Ujumuishwaji ya Kijinsia na Makundi Maalum,Vyama vya Siasa kuwa na Mipango ya kuimarisha ushiriki wa wanawake,Vijana na Watu wenye ulemavu katika Masuala ya Uchaguzi.
Na Seleman Kodima.
Bado tunaendelea kuangazia Miswada mitatu ya Sheria yaliyowasilishwa Bungeni Wiki iliyopita kabla ya Bunge kuhairishwa .
Miswada hiyo ni pamoja na wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2023, muswada wa Sheria ya Tume ya Uchaguzi wa mwaka 2023 na muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria za Vyama vya Siasa wa Mwaka 2023.
Leo tunapata maaoni ya Mhadhiri wa Chuo kikuu Huria Dkt Victoria Lihiru amesema yapo mambo mazuri waliyobaini baada ya Miswada hiyo kuwasilishwa Bungeni ikiwa ni pamoja na vyama vya Siasa kuwa na Sera ya mambo ya Ujumuishwaji ya Kijinsia na Makundi Maalum,Vyama vya Siasa kuwa na Mipango ya kuimarisha ushiriki wa wanawake,Vijana na Watu wenye ulemavu katika Masuala ya Uchaguzi.
Amesema Suala la Tatu ni kuwa na dawati la kushughulikia masuala ya Ujumuishwaji wa wanawake ,Vijana na watu wenye Ulemavu.
Akizungumzia Mapungufu katika Sheria hizo hasa Sheria ya Vyama vya Siasa amesema ipo haja sheria hiyo kuweka kiwango cha maalum vya vyama vya siasa wanapokuwa wanachagua Viongozi wao kwa kutazama kuanzia Ngazi ya Chini hada taifa ili kuwe na mjumuisho wa wanaume na wanawake katika Mfumo wa Hamsini kwa Hamsini.