Ugumu wa maisha wapelekea wagonjwa kushindwa kufuata ushauri wa kitaalam
15 November 2023, 4:37 pm
Takwimu zinaonesha kuwa duniani kote chini ya asilimia 50 ya nchi zina será za kitaifa za kufanya mazoezi ya mwili na kati ya hizo ni asilimia 40 ndio zinazofanya kazi ni muda sasa Jamii kuwa na utamaduni wa Kufanya mazoezi ili kuepukana na magonjwa yasiyo yakuambukiza .
Na Aisha Alim.
Ugumu wa maisha miongoni mwa sababu zinazotajwa kwamisha mtu mwenye ugojwa wa kisukari kufuata maelekezo ya kitabibu .
Kwa Mujibu ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO inaeleza kuwa Katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2020 mpaka mwaka 2030 watu milioni 500 wanakadiriwa kuwa watakuwa wameugua magonjwa yasiyoambukiza
Kutokana na Hali hiyo Taswira ya Habari imezungumza na baadhi ya wakazi wa jiji la dodoma ili kufahamu ni kwa namna gani wanakabiliana na mtindo wa maisha ili kuepuka kupatwa na magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
Ongezeko la wagonjwa wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza ni hasara kubwa kwa uchumi wa Taifa.
Taswira ya Habari imefanya mahojiano na Dkt. Misana Yango kutoka hospital ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma ambapo amesema kuwa ugonjwa huo licha ya ugonjwa huo kupatikana kutokana na uwepo wa sukari nyingi mwilini pia hupatikana kwa njia ya kurithi
Aidha dkt. Yango amesema iwapo mgonjwa wa kisukari asipofuata maelekezo ya kitabibu upo uwezekano wa kukua kwa tatizo na kusababisha athari zaidi kiafya.