DC Mpwapwa abaini upigaji pesa za watumia maji
13 November 2023, 5:11 pm
Sera ya Maji ina inasisitiza miradi ijengwe, iendeshwe na kusimamiwa na wananchi ili ijiendeshe kwa kufanyaa matengenezo kila inapohitajika bila kutegemea ruzuku kutoka serikalini.
Na seleman Kodima.
Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa imeamua kuziunganisha jumuiya za watumia maji (CBWSO) badala ya kila mradi kuwa na jumuiya yake ili kuongeza ufanisi na uwajibikaji katika Uendeshaji wa jumuiya hizo wilayani humo.
Hii inajiri kufuatia tathmini iliyofanyika ya mwenendo wa CBWSO ambapo inaelezwa kuwa pamoja na mazuri mengi bado baadhi ya jumuiya hizo zinakabiliwa na changamoto za kiuendeshaji ikiwemo matumizi mabaya ya fedha kama anavyobainisha Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Sophia Kizigo.
Aidha Mhe Kizigo amesema endapo jumuiya hizo zitaunganishwa pamoja zitamaliza changamoto ya uendeshwaji kindugu jambo ambalo lilikua linadidimiza watumiaji wengine.
Kila mradi wa maji ulioko kijijini ni lazima usajili kisheria chombo cha watumiaji maji Lengo kuu la kuanzisha vyombo vya watumiaji maji ni kuifanya miradi imilikiwe na kusimamiwa na wananchi wenyewe ili kuhakikisha kuwa huduma ya maji inakuwa endelevu.