

7 November 2023, 3:05 pm
Kufuatia tukio hilo wazazi wametakiwa kuwa makini na watoto wasicheze katika maeneo hatarishi hususani kipindi hiki cha mvua.
Na Fred Cheti
Mtoto mwenye umri wa miaka 4 aliyefahamika kwa jina la Denis Emanuel amefariki dunia baada ya kuteleza na kudumbukia katika kisima cha maji alipokuwa akicheza kando ya kisima hicho katika kijiji cha Ilolo wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma.
Mwanaisha Bakari ambaye ni Afisa Mtendaji wa kijiji cha Ilolo anaelezea jinsi ya tukio hilo lilivyotokea huku akiitaka jamii kuacha kuchimba visima kiholela bila ya kuweka mazingira ya uzio katika visima hivyo.
Nao baadhi ya wakazi wa kijiji hicho wametoa maoni yao kufuatia tukio hilo.
Kwa upande wake Kamanda wa jeshi la Polisi wilayani Mpwapwa Aziz Ally amewataka wakazi wilayani humo kutowaacha watoto kucheza katika maeneo hatarishi hasa kipindi hiki cha Masika ili kuepuka madhara kama hayo.