Wakulima Wagomea mbolea ya Ruzuku
31 October 2023, 11:49 am
Na Mindi Joseph.
Baadhi ya wakulima wa kijiji cha Chinangali 2 Mkoani Dodoma wamegoma Kujisajili kuchukua mbolea za ruzuku zinazotolewa na Serikali kutokana na kile wanachodai zinaua Mashamba yao.
Hayo yamebainika baada ya Dodoma Tv kufika eneo hilo na kuzungumza na wakulima hao kwa Nyakati tofauti kuhusu mwamko wao katika kujisajili na uchukuaji wa mbolea ya Ruzuku .
Wakulima hao wamesema hawana imani na mbolea hiyo kama ilivyo ya samadi hali ambayo inasababisha ugumu wa kujisajili ili kupata mbolea za ruzuku.
Afisa kilimo kijiji cha chinangali 2 Bi ,Asha Sume amesema wamekuwa wakitoa elimu kwa wakulima juu ya mbolea hiyo ambapo juhudi hizo hazijazaa matunda ya kutosha katika kubadilisha fikra za wakulima za kujenga imani na mbolea hiyo.
Mamlaka ya udhibiti wa Mbolea nchini TFRA Hivi karibuni iliwataka wakulima nchini kuendelea kutumia mbolea ya Ruzuku.
Kuanzia mwaka 2003/2004, Serikali imekuwa ikitoa ruzuku kwenye kilimo kwa njia tofauti tofauti na Katika msimu wa mwaka 2022/2023 tani 650,000 za mbolea ziliagizwa kutoka nje ya nchi.