Jamii yaonywa kuepuka unyanyasaji wa kijinsia
25 October 2023, 1:46 pm
Katibu huyo amewasihi wanaume ambao wamekuwa wakipigwa na wake zao majumbani kufichua vitendo huvyo bila haya ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.
Na Bernad Magawa.
Katibu wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Bahi Paulina Deus Bupamba amekemea vikali suala la unyanyasaji wa kijinsi huku akisisitiza suala la malezi kwa watoto ili kuwa na kizazi chenye maadili bora kwa taifa Imara.
Bupamba ameyasema hayo katika kikao cha Baraza la Jumuiya ya wazazi ya chama hicho wilaya ya Bahi kilichofanyika katika Ofiza ya CCM Wilaya ya Bahi ambapo amewataka viongozi wa Jumuiya ya wazazi kuendelea kukemea mimba za utotoni pamoja na kufichua watoto wanaoteswa na mama wa kambo kwani ni mambo yanayowajengea watoto mazingira magumu na kuwakosesha haki mbalimbali.
Katibu huyo amewasihi wanaume ambao wamekuwa wakipigwa na wake zao majumbani kufichua vitendo huvyo bila haya ili sheria iweze kuchukua mkondo wake na kusema kuwa kwa kufanya hvyo wataimarisha usawa katika familia huku akihimiza suala la malezi kwa watoto bila kubagua kwani malezi ni wajibu wa kila mzazi bila kujali ni mwanao au mtoto wa jirani.
Awali, Mwenyekiti wa jumuiya hiyo Wilaya ya Bahi Bw. Yohana Mgomi aliwasisitiza viongozi hao wa jumuiya kutoka kata mbalimbali kufanya kazi kwa kushirikiana ili kuleta tija katika kutenda kazi zao huku katibu wa jumuiya hiyo wilaya ya Bahi Henry kakulwa akiwaasa kuwa na mahusiano mema katika ngazi mbalimbali za uongozi.