Wasichana wapaswa kutambua hedhi ni fahari
18 October 2023, 9:14 am
Elimu ya hedhi salama shuleni hapo imeambatana na zoezi la kugawa taulo za kike kwa wasichana hao wa shule ya msingi Nkuhungu.
Na Mariam Kasawa.
Wasichana balehe wametakiwa kutambua kuwa hedhi ni fahari ya kila mwanamke hivyo wanapaswa kuifurahia na kujua namna bora ya kujistiri.
Elimu ya hedhi salama na jinsi ya kujistiri wakati wa hedhi imetolewa leo kwa wasichana wa shule ya msingi Nkuhungu ambapo wasichana walipata wasaa wa kujibu maswali mbalimbali na kueleza ufahamu wao juu ya hedhi.
Rogathe Makupa ni mwalimu wa shule ya msingi Nkuhungu yeye alipata wasaa wa kuzungumza na wasichana hao kuhusu namna wanavyo paswa kujistiri pamoja na kujiepusha na vitendo vya ngono.
Ni kwa namna gani wasichana hawa wamekuwa wakinufaika na elimu ya hedhi salama pamoja na kupata taulo za kike huyu hapa Mratibu wa Elimu jumuishi Bi Jane Mgidange akieleza.
Uelewa wa watoto wakike juu ya hedhi salama nao haukuwa nyuma hawa hapa baadhi yao wakieleza.