Serikali kuendelea kushirikiana na wadau binafsi kuboresha elimu
11 October 2023, 9:43 am
Serikali itaendelea kushirikiana kwa karibu na Taasisi binafsi katika kuboresha Mfumo wa Elimu nchini.
Na Thadei Tesha.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda amesema Serikali itaendelea kushirikiana kwa karibu na Taasisi binafsi katika kuboresha Mfumo wa Elimu nchini.
Hayo ameyasema leo katika Mkutano wa Wakuu wa shule binafsi katika kujadili masuala mbalimbali ya kuboresha na kutatua baadhi ya changamoto zinazowakabili hususani katika mfumo wa elimu nchini.
Katika Mkutano huo ambao umehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi ,Vijana na Ajira Mhe, protabasi katambi na naibu waziri wa elimu Mh Omari Kipanga.
Awali akizungumza katika mkutano huo Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu kazi vijana na ajira Mh Protabasi Katambi ambapo amesema kuwa kupitia wizara ya vijana kazi na ajira wanao wajibu wa kuhakikisha wanatoa kipaumbele hususani katika suala la malezi na makuzi kwa watoto na vijana.
Kwa Upande wake Naibu waziri wa Elimu Mhe, Omari Kipanga ametumia fursa hiyo kuelezea wajibu wa serikali na taasisi binafsi katika kutoa elimu nchini.