Shilingi bilion 4 kujenga shule 26 za wasichana kila mkoa
20 September 2023, 5:19 pm
Hadi sasa Serikali imefanikiwa kujenga shule 449 kati ya shule 1000 ambazo zilipaswa kujengwa nchini na shule hizo zina uwezo wa kuchukua wanafunzi 400 kwa kila shule .
Na Mindi Joseph.
Shule 26 za wasichana wa masomo ya sayansi na Hisabati zinajengwa kwa kila Mkoa Nchini ili kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji wa masomo ya sanyansi katika shule za sekondari.
Bilion 4 zinatumika kwa kila Mkoa kujenga shule hizo mpya kufutia changamoto kubwa iliyopo ya masomo ya sanyansi kutopendwa na wasichana.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma utafiti na ushauri elekezi chuo kikuu cha Dodoma Prof Razack Lokina anasema semina ya leo kwa walimu inalenga kuimarisha masomo ya sayansi katika ufundishaji.
Dr Rose Matete Ndaki ya Elimu amesema Unicef wamejitolea kusaidia mafunzo kwa walimu ili kuhakikisha wanafunzi wengi wanaingia katika masomo ya Sanyansi na Hisabati.
Kwa upande wake Mratibu wa mradi wa kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP,) Dkt Mollel Meigaru ameishukuru unicef kwa mafunzo hayo kwani yanaisaidia serikali kuboresha ufundishaji na ujifunzaji.