Wazazi watakiwa kufahamu umuhimu wa maktaba kwa mtoto
20 September 2023, 2:04 pm
Maktaba ni moja ya Taasisi inayosaidia katika kuchochea maendeleo ya mtoto pindi awapo shuleni na nyumbani.
Na Khadija Ayoub.
Ili kuchochea maendeleo ya mtoto shuleni wazazi wametakiwa kuwa na utaratibu wa kuwajengea watoto wao desturi pamoja na namna bora ya ujifunzaji pindi wawapo nyumbani na shuleni.
Miongoni mwa mambo yanayosisitizwa ni pamoja na kuwajengea wanafunzi mazoea ya kujifunza ikiwemo usomaji wa vitabu.
Bi judith Lugongo ni Mkutubi wa maktaba ya mkoa wa Dodoma hapa anaelezea namna maktaba inavyochochea suala la ujifunzaji kwa watoto.
Aidha amewataka wazazi kuondoa fikra hasi juu ya utaratibu wa kwenda maktaba ambapo hapa anaeleza zaidi juu ya suala hilo.
Baadhi ya wanafunzi wanaelezeaje juu ya umuhimu wa kwenda maktaba?