Maeneo ya ukusanyaji taka jijini Dodoma yatakiwa kuboreshwa
15 September 2023, 8:25 am
Ukaguzi wa maeneo ya kuhifadhia taka ndani ya jiji la dodoma umefanywa na mkuu wa wilaya hiyo bw. Jabir shekimweri ikiwemo maeneo ya nguhungu, changombe, miyuji pamoja na eneo la chidaji sehemu ya mwisho ya kuzika taka ngumu.
Na David Kavindi.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mh. Jabir shekimweri amemuagiza mkuu wa kitengo cha usimamizi wa taka ngumu na usafi wa mazingira katika halmashauri ya jiji la dodoma kuboresha maeneo ya ukusanyaji wa taka ndani ya jiji.
Ametoa maelekezo hayo wakati akikagua maeneo ya kukusanyia taka ndani ya jiji la Dodoma ambapo amesema serikali ina wajibu wa kushirikiana na Taasisi ya Sido pamoja na wadau wa mazingira kuwezesha uchakataji wa taka kabla ya kufikishwa katika dampo kuu la chidachi.
Nae Peter Madono meneja wa dampo la chidaya jijini Dodoma amesema changamoto ya barabara na uchakavu wa mitambo imekuwa ikisababisha kushindwa kufanya kazi ya uchakataji wa taka hizo kwa ufanisi.