Wananchi waomba serikali iendelee kuwapatia elimu ya katiba
13 September 2023, 1:23 pm
Wanasheria wanayo nafasi kubwa ya kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya katiba ya nchi ili kuwaongezea uelewa wananchi waweze kutambua haki na wajibu wao.
Na Khadija Ayoub.
Wananchi Jijini Dodoma wameiomba Serikali kuendelea kutoa elimu juu ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuwaongezea uelewa juu ya haki na wajibu wao kwa Taifa.
Dodoma Tv imefanya mahojiano na baadhi ya wakazi wa jijii la Dodoma na nilianza kwa kuwauliza iwapo wanauelewa wa kutosha juu ya katiba ya Nchini.
Bi Efrasia Peragus ni Mwanasheria kutoka kituo cha sheria na haki za binadamu dodoma anasema kuwa wao kama kituo wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kuisoma na kuielewa katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Bi. Efrasia ametoa wito kwa wananchi kujenga utamaduni wa kupenda kuisoma katiba ya nchi.
Hivi karibuni rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mh. Samia Suluhu Hassan wakati akihutubia katika ufunguzi wa mkutano maalumu wa baraza la vyama vya siasa nchini alisisitiza wanachi kupatiwa elimu juu ya katiba ya nchi kabla ya kuanza kwa mchakato wa katiba mpya.