Serikali yaendelea kuchukua tahadhari kudhibiti Polio Nchini
12 September 2023, 12:26 pm
Aidha wakuu wa Mikoa, Wilaya pamoja na Viongozi mbalimbali wametakiwa kusimamia Kampeni ya Kitaifa ya chanjo ya matone pamoja na Waganga wa Mikoa kutoa chanjo hiyo kwa wakati sambamba na kutoa elimu kwa jamii.
Na Yussuph Hassan.
Serikali imeendelea kuchukuwa tahadhari mbalimbali ili kuzia ugonjwa wa polio usiingie Nchini.
Waziri wa Afya Ummy Mwalim, amesema katika kuhakikisha Tanzania inadhibiti ugonjwa wa polio, hivi karibuni itaendesha kampeni ya chanjo ya matone katika Mikoa sita Nchini.
Aidha Waziri Ummy amefafanua tofauti ya chanjo hii na chanjo nyingine za ugonjwa polio kufuatia kupatikana kwa Mgonjwa mwingine wa polio tangu Mwaka 1996.
Waziri Ummy pia ameainisha takwimu za watoto ambao hawajapata chanjo yoyote na wale waliopata chanjo moja.