Familia zatakiwa kutatua changamoto ili kujenga ustawi wa watoto
7 September 2023, 2:27 pm
Migogoro katika familia isiposuluhishwa matokeo yake ni ndoa kuvunjika, kitendo ambacho hakipendwi na jamii, na hakina faida kwa watoto wao, madhehebu ya dini, wazazi, jamaa na wategemezi wao.
Na Yussuph Hassan.
Utatuzi wa changamoto za kifamilia umetajwa kuwa ni njia bora zaidi kwa ustawi wa watoto na jamii kwa ujumla.
Ugomvi baina ya wanandoa ni kitu cha kawaida kutokana na watu hao wawili kutoka katika malezi na mazingira tofauti ya ukuaji toka wakiwa wadogo hadi watu wazima.
Wawili hao wanapoaanza kujenga mahusiano na kukaa pamoja kama familia,kuna vitu kadhaa ambavyo kila mmoja wao huvitazama tofauti na hivyo kuleta migongano. Migongano ambayo inaweza ikarekebishika kama wenza hao wataamua kuifanyia kazi na kuelewana.
Kuna vitu vingi ambavyo husababisha ugomvi na migongano ndani ya mahusiano ya mke na mume na hapa Euphrasia Peragius, Afisa Sheria Kutoka Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu anaeleza njia nzuri za kusuluhisha migogoro hiyo ya ndoa.