Wajawazito watakiwa kuzingatia chanjo ya pepopunda
6 September 2023, 12:09 pm
Kwa mujibu wa wataalamu wa Afya wanasema kuwa iwapo mama mjamzito atazikosa chanjo hizo itachangia kupata madhara makubwa na kumuathiri mtoto aliyepo tumboni huku wakishauri kufika mapema katika vituo vya Afya pale tu Mtu atakapohisi dalili za ujauzito.
Na Richald Ezekiel.
Imeelezwa kuwa ni muhimu kwa wajawazito kuzingatia chanjo ya pepopunda ili kumuhakikishia usalama wa mama pamoja na mtoto aliyepo tumboni.
wakizungumza na Dodoma TV wataalamu wa afya ya mama na mtoto kutoka kituo cha Afya Makole Jijini Dodoma akiwemo abdallha juma pamoja na vilian Ngalya wameelezea umuhimu wa chanjo hizo huku wakiwahimiza wajawazito kuto kupuuza kwani ni hatari endapo watazikosa chanjo hizo.
Baadhi ya wajawazito kutoka kituo cha Afya Makole wameelezea namna wanavyozingatia maelekezo ya wataaalmu wa Afya ikiwemo kuzingatia Matumizi ya chanjo hizo.