Maji yakwamisha muitikio wa upandaji miti
5 September 2023, 2:40 pm
Serikali pamoja na wadau mbalimbali wameendelea kuhamasisha jamii juu ya suala la upandaji wa miti ambapo kwa mujibu wa wataalam wanaeleza kuwa miti imekuwa na faida nyingi katika kutunza mazingira.
Na Diana Masai.
Pamoja najitihada mbalimbali za wadau wa mazingira ikiwemo serikali kuendelea kuhamasisha suala la upandaji wa miti bado mwitikio wa kushiriki kupanda miti hiyo unatajwa kuwa ni mdogo ndani ya jamii.
Hayo ni kwa mujibu wa wananchi wa jiji la Dodoma wakati wakizungumza na dodoma tv kuhusiana na sababu inayochangia mwitikio mdogo wa wananchi kupanda miti katika jiji la dodoma.Wamesema kuwa miongoni mwa sababu zinazo changia ni pamoja na changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji kuzidi kuwa kubwa katika jiji la Dodoma .
Dodoma Tv imewatafuta baadhi ya wauzaji wa miti jijini Dodoma akiwemo Bw. kweka kupitia kituo hiki anawasihi wananachi kupanda baadhi ya miti inayovumilia ukame huku akielezea pia hali ya biashara ilivyo kwa sasa.