Wananchi watakiwa kuacha kutupa taka ovyo katika mazingira yao
4 September 2023, 3:27 pm
Na Diana Masai.
Ili kuondokana na uchafuzi wa mazingira jamii imeaswa kuacha kutupa taka ovyo zikiwemo taka za plastiki ambazo haziozi.
Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa mtaa wa kitenge kata ya Majengo Jijini Dodoma Helswida Mhagama wakati akizungumza na Dodoma Tv ambapo amesema ataendelea kushirikiana na viongozi wengine na pamoja na wananchi ili kutokomeza uchafuzi wa mazingira.
Katika hatua Nyingine amewapongeza watu wanaojiari kupitia shughuli ya uokotaji wa makopo kwani husaidia juu ya utunzaji wa mazingira.
Dodoma tv imekutana na Bwn. Maulidi Juma ambaye anajihusisha na upandaji wa miche mbalimbali ya miti kwa kutumia makopo na hapa anatoa ushauri juu kwa wale wanaoshiriki kutupa makopo hayo bila utaratibu maalumu.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi Jijini Dodoma wamesema kuwa wanaitambua sheria juu ya kosa la utupaji wa makopo hovyo na kuchangia uchafuzi wa mazingira na kushauri uongozi wa Jiji kushirikiana na jamii kwa karibu kutokomeza vitendo hivyo.