Dodoma FM

Wananchi watakiwa kutatua changamoto zinazo sababisha msongo wa mawazo

4 September 2023, 12:32 pm

Ni vema watu kuwa wawazi katika mambo yanayowakabili ili kupatiwa msaada.Picha na VOA.

Takwimu kutoka shirika la afya Duniani WHO zinaonyesha kuwa kila mwaka watu 800,000 hupoteza maisha kwa kujiua kutokana na msongo wa mawazo huku kila baada ya sekunde 40.

Na Naima

Wananchi wametakiwa kujenga utamaduni wa kushirikishana katika kutatua changamoto mbalimbali ili kuondokana na msongo wa mawazo ambao husababisha mtu kuwa na madhara ya kiafya.

Kauli hiyo imetolewa na Emelda Mosha ambaye ni mtaalamu wa afya ya akili kutoka jijini Dodoma wakati akifanya mahojiano na Taswira ya Habari ambapo amesema ni vyema watu kuwa wawazi katika mambo yanayowakabili ili kupatiwa msaada.

Sauti ya Emelda Mosha.
Changamoto za maisha pia zinatajwa kusababisha msongo wa mawazo kwa kiasi kikubwa. Picha na VOA.

Taswira ya Habari imekutana na baadhi ya wananchi Jijini Dodoma ambapo wamesema kuwa changamoto za maisha zinachangia uwepo wa msongo wa mawazo.

Sauti za baadhi ya wananchi.