Elimu ya usalama barabarani yaendelea kutolewa kwa wananchi
30 August 2023, 3:12 pm
Ili kupunguza vitendo vya ajali za Mara kwa mara madereva na watumiaji wa barabara kwa ujumla wameendelea kuaswa kuzingatia sheria za usalama barabarani .
Na Thadei Tesha.
Ili kupunguza ajali za barabarani zinazoweza kusabababishwa na uzembe pamoja na kutokutii sheria za barabarani jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani kimeendelea kutoa elimu kwa jaii juu ya suala hilo.
Nimekutana na Koplo Ester Makali ambaye ni mwalimu wa usalama barabarani kutoka katika kikosi cha usalama barabarani trafiki makao makuu dodoma ambapo miongoni mwa majukumu anayoyafanya ni pamoja na kutoa elimu kwa watumiaji wa barabara juu ya mambo ya kuzingatia pindi wawapo barabarani.
Na hii ni njia anayotumia yeye pamoja na askati wengine wa kikosi cha usalama barabarani kufikisha elimu hii kwa abiria pamoja na watumiaji wote wa barabara kiujumla.
lakini je ni nini hasa malengo ya elimu hii kwa jamii hapa anaendelea kutueleza wa undani zaidi juu ya suala la elimu hii kwa kwa wtumiaji wote wa barabara.
Dodoma tv imefanya mahojinao na baadhi ya abiria wanaosafiri kuelekea mikoani je ni kwa namna gani wana uelewa juu ya mambo ya kuzingatia pindi wawapo katika chombo cha usafiri?