Wakazi Bihawana watakiwa kujitokeza kuhakiki taarifa za ardhi
29 August 2023, 4:00 pm
Lengo la mradi wa LTIP ni kuboresha ufanisi katika utawala wa ardhi na kuongeza usalama wa milki kwenye maeneo ya mradi.
Na Seleman Kodima.
Wakazi wa mtaa wa Bihawana kata ya Mpunguzi jijini Dodoma wametakiwa kujitokeza hapo kesho kwa ajili ya zoezi la uhakiki wa taarifa za umiliki wa ardhi.
Kupitia taarifa ya Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma imeanisha kuwa kupitia mradi wa Uboreshaji wa milki salama za ardhi wananchi wa mtaa huo wanatakiwa kuhudhuria mkutano wa hadhara utakaofanyika shule ya sekondari Bihawana kwa ajili ya uhakiki wa taarifa za umiliki wa ardhi.
Akitoa ufafanuzi juu ya taarifa hiyo Afisa habari na mawasiliano Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Magreth Lyimo anaelezea zaidi
Lengo hilo linaenda sambamba na kuongeza idadi ya miamala itokanayo na nyaraka za umiliki, kupunguza muda unaotumika kupata nyaraka za milki, kuongeza uelewa wa usalama wa milki kwa kuzingatia jinsia, kuongeza idadi ya watanzania wanaomiliki nyaraka za umiliki pamoja na kuongeza ufanisi utakaofanya wamiliki kuridhika na mchakato wa uandaaji nyaraka za umiliki.