Jamii yashauriwa kuzingatia Zaidi matumizi ya Asali
28 August 2023, 12:57 pm
Asali inafahamika kwa muda mrefu kama chakula muhimu ambacho pia kinasaidia sana katika kupambana na magonjwa mbalimbali na matatizo yatokanayo na uzee, kwa mujibu wa tafiti mpya za wataalamu wa madawa na vifaa tiba, jarida la World News limeandika kuwa Asali inauwezo mkubwa wa kutibu kama itachanganywa na Mdalasini.
Na Abraham Mtagwa.
Licha ya Upatikanaji wa Asali kuwa Mgumu kwa baadhi ya Wananchi lakini jamii imeshauriwa kutumia Zaidi.
Hayo yamefahamika baada ya Taswira ya Habari kuzungumza na baadhi ya watumiaji wa bidhaa hiyo kutoka Jijini Dodoma ambapo wamesema kuwa, Asali imekuwa na matumizi mengi ikiwemo kutumia kama chakula na tiba.
Bw. Aboutwalib Nassoro ni Mfanyabiashara wa Asali kutoka Soko la Machinga Complex Jijini Dodoma ametoa ushauri kwa Wananchi kuwa watumiaji wazuri wa Asili licha ya changamoto ya upatikanaji wake.
Aidha Taswira ya Habari imefanya mazungumzo na Bw. Beni Majangi ambaye ni Mtaalamu wa Afya kutoka kituo cha Rebohothi Jijini Dodoma, na hapa anaeleza kuhusu matumizi na faida zinazo patikana katika Asali hasa inapotumiwa kwa usahihi.
Hata hivyo, Bw. Majangi amebainisha baadhi ya hasara zinazoweza kujitokeza kutokana na matumizi yaliyozidi ya asali katika mwili.