Jamii yatakiwa kutambua umuhimu wa kunde kiafya
28 August 2023, 11:58 am
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Shirika la Kilimo na Chakula Duniani FAO, imesema zao la Kunde na vyakula vyote vya jamii ya kunde ni nafuu na vitamu huku vikiwa na kiwango kikubwa cha protini na hivyo huweza kutumiwa badala ya nyama.
Na Abraham Mtagwa.
Jamii imeshauriwa kuwa na utaratibu wa Matumizi sahihi ya zao la Kunde kutokana na zao hilo kuwa na virutubisho vingi kiafya.
Ushauri huo umetolewa na Bw. Stephano Daburu ambaye ni Mteknolojia na Mtaalamu wa Afya kutoka Jijini Dodoma ameikumbusha Jamii juu ya matumizi sahihi ya zao hilo kiafya.
Aidha, Taswira ya Habari pia imezungumza na Watumiaji mbalimbali wa zao la kunde kutoka Jijini Dodoma ambapo wamekuwa na maoni mbalimbali kuhusiana na matumizi ya zao hili .
Kwa upande wake, Deodati Masawe ambaye ni mmoja wa Wafanyabiashara wa zao la Kunde kutoka Soko Kuu la Majengo Jijini Dodoma amesema kuwa hali ya biashara ya kunde kwa sasa ni ngumu Sokoni, huku akibainisha matumizi na faida mbalimbali za zao hilo kiafya.