Vijana Nchini watakiwa kuwa na uthubutu
16 August 2023, 7:00 pm
kwa mujibu wa vijana haoa wanasema kuwa kupitia mjadala huo uliofanyika katika ukumbi wa kambarage uliopo katika jengo la hazina Jijini dodoma umetoa funzo juu ya masuala mbalimbali ikiwemo masula ya uongozi na Demokrasia nchini.
Na Thadei Tesha.
Vijana nchini wametakiwa kuwa na uthubutu katika kushiriki masuala ya kisiasa na kuwa tunu ya kuleta Demokarasia nchini.
Hayo yamesemwa na baadhi ya wawakilishi wa vijana kutoka mikoa mbalimbali nchini walioshiriki katika mdahalo wa kitaifa wa demokrasia ulioandaliwa na one young Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa kambarage uliopo hazina jijini dodoma.
Wakizungumza na kituo hiki vijana hao wamesema kuwa ni wakati wa vijana kujihamasisha wenyewe ikiwa ni pamoja na kuwa na uthubutu wa kushiriki na kuwa kama tunu ya kuleta demokrasia nchini.
Kwa upande wake Bw Vicent Huega ambaye yeye ni miongoni mwa waandaji wa mdahalo huo anatumia fursa hii kuwataka vijana ikiwemo vijana wa kike kujiingiza katika fursa za uongozi na kuachana na matazamo hasi juu ya suala la uongozi kuwa ni la watu waliobobea katika masuala ya uongozi au wazee.