Usugu wa dawa watajwa kugharimu maisha ya binadamu
14 August 2023, 4:24 pm
Inakadiriwa kuwa kama hatua madhubuti hazitachukuliwa janga hili litaua watu milioni 10 kwa mwaka ifikapo 2050 kwani tathmini iliyofanywa mwaka 2019 ilionesha uwepo na vifo vya watu takribani milioni 1.27, ambavyo vilisababishwa moja kwa moja na vimelea sugu kwa dawa.
Na Mindi Joseph.
Usugu wa vimelea dhidi ya dawa ni janga ambalo limetajwa kutishia na kugharimu idadi kubwa ya maisha ya binadamu.
Usugu wa vimelea dhidi ya dawa husababishwa na matumizi holela ya dawa dhidi ya vimelea kwa binadamu bila ushauri wa wataalamu wa afya.
Je Matumizi sahihi ya Dawa ni Nini huyu ni Emmanuel Ndejembi Mkaguzi Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA) anatufafanulia.
Nini kifanyike kukabiliana na Changamoto ya Usugu wa vimelea dhidi ya dawa Benedict Brash ni Mkaguzi Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA) anasema.