Jimbo kuu katoliki Dodoma lapokea sanamu ya Bikira Maria
10 August 2023, 12:10 pm
Kwa mujibu wa imani ya kanisa katoliki, Mama bikira maria ndiye mama wa Yesu kristo Mkombozi wa ulimwengu, ambaye ni muombezi wa kanisa ambapo baada ya kupatikana kwa uhuru wa Tanganyika mwaka 1961, Muasisi wa Taifa hili hayati Julius Kambarage Nyerere alilikabidhi chini ya mama huyu kama muombezi wa amani ya taifa.
Na. Benard Magawa.
Waumini wa kanisa katoliki Jimbo kuu katoliki Dodoma wamepokea Sanamu ya Mama Bikira maria kutoka Jimbo la Singida kwaajili ya kuitembeza katika jimbo kuu katoliki la Dodoma kwa lengo la kuamsha imani ya waumini wa kanisa hilo pamoja na kuombea amani ya taifa,
Kuomba Mungu aepushe madhira yote mabaya yanayolikumba taifa letu yakiwa ni pamoja na ndoa za jinsia moja na utoaji wa mimba.
Ni mapokezi ya heshimakwa mama Maria yaliyofanyika Parokia ya Kintinku wilaya ya Manyoni Mpakani mwa Jimbo la singida na Dodoma, akizungumza wakati wa Mapokezi hayo Paroko wa Parokia ya Manyoni Padri Wambura akimuwakilisha Askofu wa Jimbo la singida amewakumbusha waumini kuendelea kumuomba mama maria katika shida mbalimbali walizonazo.
Kwa upande wake, Makamu wa Askofu Jimbo kuu katoliki Dodoma Padri Michael Gaula ameeleza umuhimu wa kanisa katoliki katika kumtegemea mama maria huku Paroko wa Parokia ya Bahi Padri Levocatus Majuto akitoa neno la shukrani.